Korir: Wanariadha wa Kenya Rio ni wasafi
Huwezi kusikiliza tena

Korir: Wanariadha wa Kenya Olimpiki Rio ni wasafi

Nahodha wa timu ya Kenya, Wesley Korir, amesema wanariadha wote wa Kenya walioko Rio de Janeiro kwa michezo ya Olimpiki hawajatumia dawa za kuongeza nguvu baada ya wote kupimwa na kupatikana bila hatia.

Kwa miaka ya hivi karibuni baadhi ya wanariadha wa Kenya wamefungiwa kwa kutumia dawa za kuongeza nguvu.

John Nene amezungumza na Wesley Korir mjini Eldoret eneo la Bonde la Ufa.