Maadhimisho ya mauaji ya mweusi Marekani

Waandamanaji walijizuia na magari risasi zilipofyatuliwa Ferguson, Missouri Haki miliki ya picha AP
Image caption Waandamanaji walijizuia na magari risasi zilipofyatuliwa

Kumekuwa na ufyatulianaji wa risasi katika maandamano huko Ferguson jimbo la Missouri nchini Marekani kuadhimisha mwaka wa pili wa kifo cha Michael Brown,kijana mweusi aliyepigwa risasi na polisi mzungu.

Milio ya risasi ilisikika baada ya mtu mmoja aliyekuwa akiandamana kugongwa na gari ambalo lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi.

Ufyatulianaji huo ulitokea muda mchache baada ya kwanza kwa maadhimisho ya pili ya mauaji ya kijana huyo mweusi.

Mauji ya Michael Brown yalizua ghasia na mjadala nchini humo kuhusu utumiaji wa nguvu kupitia kiasi unaotekelezwa na polisi dhidi ya watu weusi.

Maandamano dhidi ya mauaji ya vijana weusi mikononi mwa polisi wazungu yalienea hadi katika miji mingine.

Mauji hayo vilevile yaliyochochea kuanzishwa kwa vuguvugu la Black Lives Matter ilikuangazia masaibu ya wanaume weusi mikononi mwa polisi.

Hakuna aliyejeruhiwa kufuatia ufyatulianaji huo.

Haki miliki ya picha Other
Image caption Maandamano huko Ferguson jimbo la Missouri nchini Marekani kuadhimisha mwaka wa pili wa kifo cha Michael Brown,kijana mweusi aliyepigwa risasi na polisi mzungu.

Sharon Cowan aliiambia shirika la habari la AP kuwa gari lililomgonga lilikuwa likiendeshwa kwa kasi na mwanamke.

Video za tukio hilo zinamuonesha Cowan akiwa amelala chini kisha waandamanaji wanalifuata gari hilo.

Punde baadhi yao walichomoa bastola na kulifyatulia risasi.

Afisa mkuu wa Polisi katika mji wa Ferguson Jeff Small anasema kuwa dereva huyo anashirikiana na polisi na kuwa ameonesha dalili kuwa hakukusudia kumgonga mwandamanaji huyo.

Awali babake mhasiriwa Michael Brown aliwaasa waandamanaji kwa kusema kuwa sharti ulimwengu ufahamu wazi kuwa sio haki vitendo vinavyofanyiwa weusi.

''rangi nyeusi inavutia'' alisikika akisema.