Msomali kuwa mbunge wa Minnesota Marekani

Bi Ilhan Omar aliyezaliwa Somalia anawania kuwa mbunge Minnesota

Chanzo cha picha, StarTribune

Maelezo ya picha,

Bi Ilhan Omar aliyezaliwa Somalia anawania kuwa mbunge Minnesota

Mwanamke mmoja aliyezaliwa Somalia lakini sasa ni mpiganiaji haki za kibinadamu Ilhan Omar anapigiwa upatu kuweka historia kuwa Mmarekani wa kwanza mzaliwa wa taifa hilo la Afrika Mashariki kuchaguliwa kuwa mbunge nchini Marekani.

Binti huyo mwenye umri wa miaka 33 amemuangusha mbunge aliyehudumu kwa zaidi ya mika 44 katika bunge la jimbo la kwa chama cha Democratic .

Mbunge huyo wa zamani bi Phyllis Kahn amekuwa akiiwakilisha DFL, kinachoshirikiana na chama cha Democratic .

Bi Omar, na familia yake walitoroka mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia kwenda Kenya walikoishi kwa miaka minne kabla ya kwenda Marekani.

Huko walihamia eneo lenye wasomali wengi la Cedar-Riverside, katika jimbo la Minnesota.

Kizingiti kilichosalia mbele ya bi Omar ni mpinzani wake wa chama cha Republican Abdimalik Askar, ambaye pia ni msomali raia wa Marekani katika uchaguzi mkuu ujao ulioratibiwa kufanyika mwezi Novemba.

Hiyo inamaanisha iwapo kila hali itasalia ilivyo basi Msomali mmoja raia wa Marekani atakuwa bungeni mwakani.