Kobe amchanganya mmliki wake Uingereza

Kobe huyo aitwaye Zuma alitambaa na kuingia kwenye mifuko ya taka.
Image caption Kobe huyo aitwaye Zuma alitambaa na kuingia kwenye mifuko ya taka.

Nchini Uingereza kobe mmoja wa miaka tisa ametenganishwa na mmiliki wake baada ya kupakizwa kwenye gari la taka hadi sehemu ya kuhifadhia uchafu pasipo kujua.

Kobe huyo aitwaye Zuma alitambaa na kuingia kwenye mifuko ya taka.

Mmliki wake Sara Joiner alishindwa kukisia mahali alipopelekwa na kuamua kupiga simu kwa hasira kwa maofisa wa Westminster mjini London.

Maafisa hao walipekua maelfu ya mifuko ya uchafu na kunasa mguu huku akiwa na masoneneko.

Zuma kwa sasa ana furaha ya kurudishwa kwenye bustani yake baada ya masaa kadhaa ya kutoroka.