WikiLeaks: Julian Assange kuhojiwa na maafisa wa Sweden

Julian Assange Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sweden imekuwa ikitaka Assange arejeshwe nchini humo kujibu mashtaka

Serikali ya Ecuador imesema imefikia makubaliano na serikali ya Sweden kuwezesha maafisa wa Sweden kumhoji mwanzilishi wa mtandao wa WikiLeaks Julian Assange.

Mahojiano hayo yatafanyika katika ubalozi wa Ecuador jijini London, ambapo Assange aliomba hifadhi na amekuwa akiishi kwa miaka minne iliyopita.

Hilo litafanyika katika kipindi cha wiki chache zijazo, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Jumatano na wizara ya mambo ya nje ya Ecuador.

Julian Assange anakabiliwa na tuhuma za ubakaji na unyanyasaji wa kingono nchini Sweden.

Amekanusha madai hayo na anasema hicho ni kisingizio cha kutaka kumpeleka Marekani, taifa linalotaka kumhoji kuhusiana na shughuli za Wikileaks, shirika lililofichua siri nyingi za Marekani.