Uingereza: Wanafunzi wa kike wana matatizo ya akili zaidi

Zaidi ya theluthi moja ya wanafunzi wa kike 'wana maradhi ya kiakili'

Haki miliki ya picha LEKCEJ
Image caption Msongo wa mawazo lilibainika kuwa ndio tatizo kubwa miongoni mwa wanafunzi wa kike

Mmoja kati ya wanafunzi wa kike watatu nchini Uingereza ana maradhi ya kiakili, Uchunguzi umebaini.

Hii ililinganishwa na takriban wanaume watano wanaosoma masomo ya shahada, utafiti uliofanywa na the YouGov miongoni mwa wanafunzi 1,061 ulibaini.

Kwa ujumla, asilimia 27% ya wanafunzi walisema walikua na matatizo ya afya ya akili. Idadi hiyo ilipanda miongoni mwa wanafunzi wapenzi wa jinsia moja wa kike na wakiume kwa kiwango cha asilimia 45%, walio na hisia za jinsia tofauti na wale walio na hisia za jinsia zote mbili.

Vyuo vikuu nchini Uingereza vimesema kuwa vinafanya jitihada kubwa kuboresha huduma ambazo za kuwasaidia wanafunzi wenye matatizo hayo

Kati ya wanafunzi waliokiri kuwa wana matatizo ya kiakili:

  • 77% walikua na msongo wa mawazo
  • 74% walikua na mfadhaiko

Mnamo mwezi Mei , takwimu zilizochapishwa na shirika la ONS zilionyesha kuwa visa vya kujiua miongoni mwa wanafuzi vilioongezeka kwa kiwango cha juu kuwahi tangu kutangazwa kwa mara ya kwanza kwa takwimu za visa hivyo mwaka 2007.

Takwimu hizi za mwaka 2014 zilionyesha kuwepo kwa visa 130 vya kujiua England na Wales miongoni mwa wanafunzi wanaoishi shuleni wenye umri wa kuanzia miaka 18 ama zaidi. Kati ya hao, vifo 97 vilikua vya wa kiume na 33 walikua wa kike.

Kumekua na hofu juu ya viwango vya utoaji wa huduma za matatizo ya kiakili zitolewazo na vyuo vikuu.

Lakini utafiti unaonyesha wanafunzi wana uelewa mkubwa kuhusu huduma za matatizo ya akili zitolewazo na vyuo .

________________________________________