KFC yaonywa isiuze kuku waliotibiwa na antibiotiki

KFC

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

KFC yaonywa isiuze kuku waliotibiwa na antibiotiki

Kampuni inayomiliki maduka ya Kentucky Fried Chicken KFC imeonywa ikome kuchinja kuku waliotibiwa kwa madawa ya kiuavijasumu au antibiotiki.

Mashirika yanayowakilisha makundi ya wanunuzi wa bidhaa 350,000 nchini Marekani wamewasilisha mapendekezo hayo kwa kampuni ya inayomiliki Kentucky Fried Chicken Yum Brands kufuatia malalamishi kuibuka madawa hayo yanaathiri siha ya walaji wake.

Tayari KFC imeahidi kupunguza matumizi ya madawa hayo ya binadamu kwa kuku kuanzia mwaka ujao.

Wanaharakati wanadai kuwa sera nchini Marekani zinaruhusu matumizi ya dosi ya binadamu kwa kuku jambo ambalo kimsingi linawafanya walaji wa kuku hao kumeza dozi ya Antibiotiki ambayo hawakukusudia.

Dawa hizo za antibiotiki hutumika na wafugaji wa kuku ilikuimarisha kasi ya kukua ya kuku wao iliwatimize vigezo vya uzani na hivyo faida kubwa katika muda mchache.

Msemaji wa KFC amesema kuwa wanatathmini athari iliyopo kwa wateja wao kabla ya kutoa vigezo vipya vya kuimarisha ubora wa kuku watakaowachinja.

Bi Lena Brook wa shirika la wanunuzi la Natural Resources Defense Council, anasema kuwa KFC sharti ikaze buti kwani vyakula vyao vinaathiri afya ya wateja wao.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Maduka mengine yanayomilikiwa na Yum , Taco Bell na Pizza Hut -yanaazimia kupunguza ununuzi wa kuku hao waliotibiwa na antibiotiki.

Maduka mengine yanayomilikiwa na Yum , Taco Bell na Pizza Hut -yanaazimia kupunguza ununuzi wa kuku hao waliotibiwa na antibiotiki.

Juma lililopita maduka ya McDonald yalipiga marufuku ununuzi wa kuku zilizotibiwa na antibiotiki.