UN kuchunguza mauaji Oromia na Amharia Ethiopia

Watu kadhaa wameuawa kufuatia makabiliano baina ya polisi na waandamanaji
Maelezo ya picha,

Ramani ya Ethiopia

Umoja wa mataifa unataka Ethiopia kuruhusu waangalizi wa kimataifa kuingia katika maeneo ambayo hivi majuzi yaliathirika na maandamano yenye ghasia nchini humo.

Mkuu wa shirika la haki za binadamu laumoja wa mataifa Zeid Ra'ad Al Hussein anasema hakujakuwa na jaribio la kuchunguza ghasia hizo au kumpata mhusika.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Maelfu ya watu waliandamana dhidi ya sera ya serikali kuwapokonya ardhi

Shirika la haki za binadamu la kimataifa Amnesty International linasema kuwa takriban watu 100 waliuawa kwenye maandamano katika maeneo ya Oromia na Amhara mwishoni mwa wiki.

Maelezo ya picha,

Waethiopia wazika waliouawa katika maandamano

Jumapili ilishuhudia makabiliano makali baina ya waandamanaji na maafisa wa utawala.

Waandamanaji hao walikuwa wakipinga sera mpya ya serikali ya kupanua jiji la Addis Ababa ambayo ililazimu baadhi yao kupokonywa ardhi.

Kulishuhudiwa pia maandamano makubwa katika eneo la Oromia ambako kunaaminika kuwa watu kadhaa waliuawa.