Madaktari wa Mumbai mashakani kwa kuuza figo

Uuzaji wa figo India
Maelezo ya picha,

Uhaba wa viungo ambavyo binadamu wanaweza kupeana umechochea mauzo ya siri ya viungo kote nchini India

Polisi nchini India wamewashtaki madaktari watano makosa yenye uhusiano na biashara ya pigo ya binadamu.Maafisa wa polisi wanasema madaktari hao walihuska katika kisa kimoja ambapo walihusika katika kutoa figo ya binadamu kinyume cha sheria katika Hospitali ya Hiranandani iliyopo magharibi mwa mji wa Mumbai.

Polisi walichunguza hospitali baada ya taarifa kuenea kwamba watu maskini, wengi wao kutoka maeneo ya vijijini, wamekua wakilipwa kuuza figo zao.

Figo jingine lilitolewa kwa binadamu mwezi Juni katika hospitari maarufu mjini Delhi.

Naibu kamishna wa polisi wa Mumbai, Ashok Dudhe, amesema kuwa madaktari walishtakiwa kwasababu "hawakufuata taratibu zilizopo".

"siku mbili zilizopita tulipata ripoti kutoka kwa mkurugenzi wa huduma za afya wa Mumbai. Katika ripoti hii kulikua na mashtaka yaliyotolewa dhidi yamadaktari hawa kama vile uzembe chini ya sheria ya mwaka 1994 ya upasuaji wa viungo vya binadam ," shirika la habari la Reuters lilimkariri Bw Dudhe akielezea.

Aliongeza kusema kuwa watu 14, akiwemo mtoaji wa figo, mpokeaji na aliewakutanisha, wamekamatwa kwa sasa.

Polisi walianza kufanya uchunguzi wa hospitali baada ya wahudumu wake kuwafahamisha kuhusu visa walivyovishuku vya upasuaji wa figo.

Ni wanafamilia pekee wanaoweza kujitolea kutoa viungo vya mwili kwa wagonjwa nchini India, na biashara yoyote ile ya viungo ni kinyume cha sheria.

Hata hivyo uhaba wa viungo vinavyoweza kuhamishwa kutoka kwa mtu mmoja kuelekea mwingine unachochea kushamiri mauzo ya siri ya viungo vya mwili kote nchini India.