Mwanasheria nchini Canada asikitishwa na mauaji ya mteja wake

Alieleza kuwa bwana Driver alikuwa mmoja wa wateja wake, kwa sababu alikuwa anaheshimika
Image caption Alieleza kuwa bwana Driver alikuwa mmoja wa wateja wake, kwa sababu alikuwa anaheshimika

Mwanasheria wa mshukiwa wa ugaidi nchini Canada, ameiambia BBC kuwa ameshtushwa kusikia mteja wake amepigwa risasi wakati wa operasheni ya polisi wa Ontario katika mji wa Strathroy.

Leonard Tailleur anayemwakilisha Aaron Driver ambaye ni marehemu, alijulikana kwa kuwahurumia waislam, alipohukumiwa mwezi wa Februari.

Bwana Tailleur amesema kumekuwa na pingamizi juu yake ili kumlinda na kujihusisha na wanaharakati wa kiislam sambamba na kuulizwa maswali kedekede.

Image caption Polisi wanasema Aaron Driver pichani alikuwa anahusishwa na matukio kadhaa ya kigaidi

Alieleza kuwa bwana Driver alikuwa mmoja wa wateja wake, kwa sababu alikuwa anaheshimika.

Polisi wamesema wana taarifa sahihi kuhusu wanaotuhumiwa na mabomu ya kujitoa mhanga.

Image caption Polisi wenye silaha walionekana katika mji wa Strathroy yalipokuwa makazi ya Driver

Familia yake imeliambia shirika la utangazaji la CBC kuwa Driver alipigwa risasi baada ya kuwasha kifaa ambacho kilimjeruhi yeye sambamba na mtu mwingine.