Nyota wa Bollywood Rukh Khan akamatwa Marekani

Shah Rukh Khan

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Si mara ya kwanza kwa Shah Rukh Khan kukamatwa katika viwanja vya ndege vya Marekan

Nyota huyo wa filamu za Bollywood Shah Rukh Khan ameelezea kusikitishwa na kitendo cha "kukamatwa" na mamlaka za Marekani katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles.

Shah Rukh Khan aliwahi kuweka aliwahi kuweka mahabusu kwenye viwanja vya ndege vya Marekani awali.

Haijafahamika wazi ni kwa nini Khan alitiwa nguvuni, na kwa muda gani.

Balozi wa Marekani nchini India ameomba msamaha kwa kukamatwa kwa Khan na amesema kuwa mamlaka zinafanya kila liwezekanalo kuhakikisha tukio kama hilo halitokei tena.

Mnamo mwaka 2012, Khan alikamatwa na kushikiliwa kwenye uwanja wa ndege wa White Plains karibu na jiji la New York kwa dakika 90.

Mwaka 2009, alizuiliwa kwa muda wa saa mbili katika wanja wa ndege wa Newark.

Aliachiliwa baada ya ubalozi wa India kuingilia kati.

Khan, ambae aliwasili Los Angeles Ijumaa, aliandika kwenye ukurasa wake wa Tweeter: '' Ninaelewa kikamilifu jinsi hali ya usalama wa Marekani na dunia ulivyo. Lakini kukamatwa kwenye idara ya uhamiaji ya Marekani kila wakati inaudhi sana''.