Cannes yapiga marufuku uvaaji wa bikini inayohusishwa na ugaidi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanamke aliyevalia vazi la kuogelea lililofunika mwili mzima akitembea ufukweni nchini Ufaransa.

Wanawake wanaovalia mavazi yakuogelea aina ya bikini watatakiwa kuyabadilisha kuwa katika vazi la "heshma "

Meya wa Cannes kusini mwa Ufaransa amepiga marufuku mavazi la kuogelea yanafunika mwili mzima maarufu "burkini" kuvaliwa maeneo ya ufukweni, kutokana na hofu ya umma.

David Lisnard amesema mavazi hayo ni " Ishara ya itikadi kali za kiislam" na yanaweza kuzusha wasi wasi wakati huu ambapo Ufaransa inalengwa na mashambulio ya waislam.

Ufaransa imekuwa katika hali ya tahadhari kufuatia msururu wa visa vya mashambulio likiwemo shambulio la lori katika mji wa karibu wa Nice.

Yeyote anaepatikana akikiuka sheria mpya anaweza kukabiliwa na faini ya Euro 33.

Kwanza awataombwa kubadilisha na kuvalia vazi jingine la kuogelea ama waondoke.

Hakuna yeyote aliyewahi kukamatwa kw aukiukaji wa sheria ya uvaaji wa bikini Cannes tangu ilipoanza kutekelezwa mwisho ni mwa mwezi wa Julai.

Hii sio mara ya kwanza kwa wanawake kuwekewa masharti ya nguo nchini Ufaransa.

"mtu yeyote alievalia mavazi yaliyo kinyume na maadili haruhusiwi kwenda maeneo ya ufukweni ama maeneo ya kuogelea''.

"mavazi ya ufukweni yanayoonyesha mtu ni wa dini fulani , wakati Ufaransa na maeneo ya kuabudu yanalengwa na mashambulio ya ugaidi , inaweza kusababisha hatari miongoni mwa umma ."

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES
Image caption A burkini (ikionyeshwa inavyovaliwa kushoto) na kulia (muogeleaji wa Ufarasa Pascal Pichon)akionyesha vazi la mashindano ya kuogelea

Maafisa watatakiwa kutofautisha baina ya mavazi ya kuogelea ya bikini na yale yanayofaa.

Mwaka 2011 ilikua nchi ya kwanza barani Ulaya kuzuia vazi linalofunika uso mzima la kiislam, linalofahamika kama burka pamoja na lile linalofunika sehemu ya uso- niqab.

Mapema wiki hii utawala katika maji yanayomilikiwa na mtu binafsi karibu na mji wa Marseille ulizuia uvaaji wa bikini siku moja baada ya kukabiliwa na ukosoaji.

Muungano wa wanaharakati wa haki za binadamu (LDH) umesema utapinga marufuku hiyo mahakamani.