Afrika kwa Picha: 5 - 11 Agosti 2016
Huu hapa ni mkusanyiko wa picha za matukio muhimu barani Afrika, na picha za Waafrika kutoka maeneo mengine ulimwenguni, wiki hii.

Chanzo cha picha, EPA
Yemi Geoffrey Apithy (katikati) abeba bendera ya Benin katika uwanja wa Maracana, wakati wa ufunguzi wa michezo ya olimpiki mjini Rio de Janeiro, Brazil, Ijumaa.
Chanzo cha picha, Reuters
Bondia wa Cameroon Wilfred Seyi Ntsengue, asherehekea ushindi wake katika kitengo cha uzani wa kati (kilo 75) kwa wanaume, Jumanne.
Chanzo cha picha, Reuters
Chuma yamzidi nguvu! Raia wa Cameroon Sonkbou Foudji akishiriki michezo ya kunyanyua vyuma, katika kitengo cha uzani wa kilo 69 kwa wanawake.
Chanzo cha picha, AFP
Wachezaji wa timu ya Kenya ya raga kwa watu saba kila upande washerehekea pamoja na mashabiki, hata baada ya kushindwa na Japan, 31-7, katika Olimpiki mjini Rio, uwanja wa Deodoro.
Chanzo cha picha, AP
Tabasamu Rio! Msichana mdogo, shabiki wa timu ya voliboli ya Cameroon atabasamu kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya Cameroon na Japan kwa wanawake siku ya Jumatatu.
Chanzo cha picha, EPA
Alexandre Bouzaid raia wa Senegal aanguka wakati wa mchuano wa vitara dhidi ya raia wa Hungury siku ya Jumatano. Hatimaye Alexandre alishindwa na Boczko Gabor wa Hungury kwa pointi 15-9.
Chanzo cha picha, EPA
Kutoka Rio, hadi Zimbabwe. Mwanajeshi aongoza wanajeshi wengine wakati wa maadhimisho ya siku ya wanajeshi wa Zimbabwe siku ya Jumatano, mbele ya rais wa taifa hilo Robert Mugabe.
Chanzo cha picha, Reuters
Wafuasi wa rasi wa Zambia Edgar Lungu, na chama chake cha PF wawasili mjini Lusaka, kuhudhuria mkutano wa kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu siku ya Jumatano.
Chanzo cha picha, AFP
Mwaniaji wa urais wa chama kikuu cha upinzani, Hakainde Hichilema pia alifanya mkutano wake wa mwisho mjini Lusaka siku iyo hiyo. Ushindani mkali unatarajiwa kati ya rais Edgar Lungu, na Hakainde Hichilema.
Chanzo cha picha, Reuters
Zoezi la uchaguzi lilikuwa la amani na watu wengi walishiriki. Raia wa Zambia walipiga kura tano - ya urais, wabunge, mameya, madiwani na ya marekebisho ya kitengo cha haki za binadam kwenye katiba ya taifa hilo.