Zaidi ya raia wa Sudan Kusini 110,000 walitorokea Uganda

Wakimbizi wa Sudan Kusini

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

robo tatu ya wakimbizi waliokimbilia Uganda waliwasili yalipoibuka mapigano ya mwezi uliopita

Shirika la Umoja wa mataifa la huduma kwa wakimbizi linasema kuwa takriban watu 110,000 wamekimbilia nchini Uganda kutoka taifa jirani la Sudan Kusini mwaka huu.

Linasema robo tatu ya wakimbizi hao waliwasili tangu yalipoibuka mapigano mapya ya mwezi uliopita.

Uganda inahangaika kukabiliana na wimbi hilo. Wakati mwingine vituo vya kupokelea wakimbizi hupokea mara tano ya idadi inayopaswa kupokelewa.

Umoja wa mataifa umesema matatizo ya kiuchumi Sudan Kusini, kunakosababisha mfumuko wa bei za bidhaa na kushuka kwa thamani ya sarafu ya nchi kwa asilimia 600%, inaongezea hali ya mzozo huo.