Waasi wa Syria wafunga njia ya IS ya kukwepa mapigano

Mapigano Syria Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiganaji wa vikosi vya Syrian Democratic Forces wakiwaongoza raia kuelekea mahala salama

Wapiganaji wa kiarabu wa jamii ya Kikurdi na wale wa kiarabu wanasema kuwa wameukomboa mji wa kaskazini mwa Syria wa Manbij kutoka kwa wapiganaji wa Islamic State, na kufunga bara bara yao ya kuelekea Ulaya.

Muungano huo wapiganaji ulipigana kwa muda wa saa 73 kuwaondosha IS na unasema kuwa umewatorosha raia 2,000 waliokua wakitumiwa kama ngao ya kivita katika siku ya mwisho ya mapigano.

IS liliuteka mji wa Manbij, ulioko karibu na mpaka na Uturuki miaka miwili iliyopita.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Wapiganaji wakiwaliwaza raia waliokombolewa kutoka mji wa Manbij
Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Wakina mama wenye watoto wachanga ni miongoni mwa wale waliokombolewa

Bara bara za kuelekea katika mji unaokabiliwa na mapigano na wa pili kwa ukubwa nchini Syria, Aleppo, na mji mkuu wa IS, Raqqa, zinapita katika mji wa Manbij.

"baada ya kukomboa mji wa Manbij, wafuasi wa IS hawataweza kusafiri kwa uhuru kwenda na kutoka Ulaya tena ,"alisema kiongozi wa wakurdi wa Syria Salih Muslim.

Vikosi vya muungano wa Syrian Democratic Forces (SDF) vinajumuisha wanamgambo wa kundi la wanamgambo wa Kikurdi YPG lenye nguvu.

Katika mapigano yao walisaidiwa na mashambulio ya anga ya vikosi vinavyoingozwa na Marekani katika maeneo yanayodhibitiwa na IS.