Mgombea wa upinzani Zambia Hakainde Hichilema anaongoza

Hakainde Hichilema Haki miliki ya picha AFP
Image caption Hakainde Hichilema anaongoza dhidi ya mpinzani wake rais wa sasa Edgar lungu kwa kura zaidi ya elfu sita

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais nchini Zambia yanaonyesha kuwa mgombea wa chama kikuu cha upinzani, Hakainde Hichilema anaongoza kwa ushindi wa kura chache.

Takwimu za Tume ya uchaguzi zinaonyesha Bw Hichilema yuko mpele ya Edgar Lungu rais wa sasa wa zambia kwa kura zaidi ya elfu sita.

Tume ya Uchaguzi ya Zambia ilipinga shutuma kutoka kwa Bw Hichilema kwamba ilikula njama na serikali ya kuchelewesha kutangaza matokeo ya uchaguzi.

Ilisema ushiriki wa wapiga kura zaidi ya asilimia hamsina na saba unamaanisha kwamba shughuli ya kuhesabu kura itachukua muda kuliko ilivyo tarajiwa.

Edgar Lungu alichaguliwa mwaka jana kwa ushindi mdogo kufuatia kifo cha rais aliekuwepo mamlakani wakati huo, Michael Sata