Uingereza: Waliokua na saratani waliweza kuwasaidia watu viungo vya mwili

Msaada wa viungo vya mwili Haki miliki ya picha SPL
Image caption Macho ni moja ya viungo ambavyo watu wenye saratani waliweza kuwasaidia wenzao kama msaada.

Mamia ya watu nchini Uingereza wamepokea viungo vya mwili kutoka kwa mtu aliewahi kuwa na historia ya saratani, licha ya kwamba wengi huamini kwamba huwezi kumsaidia mtu kiungo cha mwili kama una maradhi ya saratani.

Jumla ya watu 272 waliofanyiwa upasuaji wa kutolewa viungo vya mwili kwa ajili ya kuwasaidia wenzao nchini Uingereza katika kipindi cha miaka mitano iliyopita walikua na historia ya saratani , kwa mujibu wa takwimu zilizobainiwa na shirika la habari la Press Association.

Usaidizi wa viungo vyao uliwezesha watu 675 kupokea tiba ya upasuaji wa kupokea viungo vya mwili.

Macho ni moja ya viungo ambavyo watu hao waliweza kuwasaidia wenzao.

Takwimu kutoka huduma za kituo cha NHS Blood na Transplant pia ulionyesha kwamba watu 1,033 ambao waliugua aina fulani ya saratani walikwenda kutoa msada wa macho - lakini si viungo vingine.

Maafisa wanasema kuwa kuna ''dhana potofu'' kwamba watu wenye saratani hawawezi kutoa msaada wa viungo vyao. Lakini katika hali fulani ni jambo inawezekana.