Watoto pacha walioshikana wazaliwa Syria

Nawras na Moaz

Chanzo cha picha, SYRIAN ARAB RED CRESCENT

Maelezo ya picha,

Nawras na Moaz

Mwanamke mmoja amejifungua watoto mapacha walioshikana nchini Syria ambapo kumeshuhudia vita vikali.

Nawras na Moaz, walizawa wakiwa wameshikana kwenye kifua na utumbo wao ukiwa nje, katika mji wa Douma mwezi Julai.

Chanzo cha picha, SYRIAN ARAB RED CRESCENT

Maelezo ya picha,

Nawras na Moaz wakipokea matibabu

Watoto hao wamesafirishwa kwa gari la kuwabebea wagonjwa na kupelekwa katika hospitali ya watoto karibu na mji wa Damascus.

Madaktari wa Syria wameomba msaada kutoka kwa Shirika la Afya Duniani (WHO), wakisema kwamba iwapo watoto hao hawatafanyiwa upasuaji watafariki. .

Pacha hao wamesafiri pamoja na mama yao na shangazi yao na imesemekana watoto hao wako katika hali nzuri.