Edgar Lungu aongoza matokeo ya awali Zambia

Wapiga kura na kadi zao
Image caption Foleni ndefu zilishuhudiwa katika vituo vingi vya kupigia kura

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa urais nchini Zambia yanaonesha Rais Edgar Lungu kwa sasa anaongoza.

Kufikia sasa matokeo ya maeneo bunge zaidi ya 20 kati ya jumla ya maeneo 156 yametangaza matokeo.

Matokeo kamili ya uchaguzi huo yanatarajiwa baadaye Jumapili.

Kunaonekana kuwa na ushindani mkali kati ya Bw Lungu na mgombea wa upinzani Haikainde Hichilema.

Wakati mmoja, Bw Hichilema alikuwa akiongoza.

Awali, tume ya taifa ya uchaguzi ilipuuzilia mbali tuhuma kutoka kwa Bw Hichilema, kwamba tume hiyo inashirikiana na chama tawala kuchelewesha matokeo.

Huwezi kusikiliza tena
Mambo 10 muhimu kuhusu uchaguzi Zambia

Edgar Lungu alichaguliwa kuwa rais mwaka jana kufuatia kifo cha rais wa wakati huo Michael Sata.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii