Wanamgambo wa IS wadhibitiwa Iraq

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mapigano yameendelea Mosul kabla ya operesheni dhidi ya wanamgambo wa IS

Vikosi vya Kikurdi nchini Iraq vimesema vimedhibiti Vijiji kadhaa karibu na mji wa Mosul kutoka kwenye himaya ya wanamgambo wa Isalamic State, mji mkuu ambao unashikiliwa na wanamgambo nchini humo.

Mapambano yalianza alfajiri siku ya Jumapili, vikosi vikisaidiwa na mshambulizi ya anga ya muungano wa majeshi yanayoongozwa na Marekani katika operesheni ya kupambana na IS.

Vikosi vya serikali ya Kikurdi na Iraq vimekuwa vikiuzingira mji wa Mosul kabla ya mapambano ya kuutwaa mji wenyewe.

Mosul, mji wa pili kwa ukubwa nchini Iraq umekuwa ukidhibitiwa na Islamic State tangu mwezi Juni mwaka 2014.

Kamanda wa majeshi ya kikurdi amesema wanajeshi zaidi ya 5,000 wako kwenye Operesheni.Mapigano bado yanaendelea.

Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa mapambano katika mji wa Mosul yanaweza kusababisha tatizo kubwa la kibinaadam duniani.