Can Dundar ajiuzulu uhariri mkuu ,Uturuki

Uturuki
Maelezo ya picha,

Can Dundar akiwa pamoja na Erderm Gul

Mmoja wa waandishi nguli nchini Uturuki , Can Dundar, ametangaza uamuzi wake wa kujiuzulu nafasi yake ya mhariri mkuu katika gazeti kuu la upinzani, Cumhuriyet.

Mnamo mwezi wa tano mwaka huu,yeye pamoja na mfanyakazi mwenziwe (Erdem Gül), walihukumiwa adhabu ya kifungo cha miaka kumi na tano jela bada ya gazeti lao kuchapisha taarifa inayowatuhumu usalama wa taifa la Uturuki kwa kuwa na Ushirika wa silaha za magendo kwa waasi wa Kiislam nchini Syria.

Baada ya taarifa hiyo wawili hao walikumbwa na hatia ya kufichua taarifa za siri za serikali.Bwana Dundar yeye aliachiliwa huru kwenda nyumbani huku akisubiri rufaa na inaaminika ameondoka nchini Uturuki.

Akifafanua hatua yake hiyo ya kujiuzulu, Dundar amesema kwamba hana imani tena na mfumo wa ki mahakama baada ya mfumo huo kushindwa katika jaribio la mapinduzi la mwezi uliopita .