Afisa wa Korea Kaskazini adaiwa kutorokea Uingereza

rais wa Korea kaskazini
Maelezo ya picha,

Rais wa Korea kaskazini

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Uingereza imesema kuwa inachunguza madai ya vyombo vya habari vya Korea Kusini kuwa afisa mmoja wa ubalozi wa Korea Kaskazini ametoroka kazi yake na kuomba hifadhi ya kisiasa nchini Uingereza.

Kulingana na vyombo vya habari vya Korea Kusini ametoroka kutokana na kushinikizwa vikali na Serikali yake kupambana na ukosoaji unaotolewa kwa Serikali yake.

Korea Kaskazini ina ubalozi Magharibi mwa jiji la London.

Maafisa wa kibalozi katika afisi zao ni wachangamfu, hasa katika maduka yao chakula chao cha asili wakati wa mlo wa jioni.

Watoto wao wanahudhuria masomo katika shule za kitaifa na mmoja ya mchezaji mahiri wa tenisi. Wakati mwingine afisa huyo hucheza golfu.

Hata hivyo katika upande mwingine wa maisha yao, wanatumia wakati wao mwingi kuwachunguza wakimbizi wengi kutoka Korea Kaskazini. Wakimbizi wengi wanaishi katika eneo la New Malden London Kusini.

Maafisa wawili pengine ni wale waliojitokeza katika kinyozi kimoja na kulalamikia picha ya kiongozi wa Korea Kaskazini iliyokuwa na maneno kwamba siku ya kuwa na nywele mbovu.

Maafisa hao pia walionekana kumsindikiza kaka wa kiongozi wao hadi maonyesha ya muziki katika Albert Hall jijini London.

Vyombo vya habari vya Korea Kusini vimeanza kuchunguza kazi ya kichini chini inayotekelezwa na maafisa hao wa Korea Kaskazini jijini London.