Ndege za Urusi kuruka kutokea Iran

Ndege za kivita za Urusi zimeanza kwa mara kwanza kutumia ngome yake ya ndege za kijeshi iliyopo Iran Haki miliki ya picha AP
Image caption Ndege za kivita za Urusi zimeanza kwa mara kwanza kutumia ngome yake ya ndege za kijeshi iliyopo Iran

Ndege za kivita za Urusi zimeanza kwa mara kwanza kutumia ngome yake ya ndege za kijeshi iliyopo Iran kuwashambulia waasi nchini Syria.

Hii ni mara ya kwanza Urusi inatekeleza harakati zake za kijeshi kupitia Iran tangu vita kuu ya pili ya dunia.

Waziri wa Ulinzi wa Urusi anasema makombora ya masafa marefu na ndege za kivita zimepaa kutokea ngome yake ya kijeshi iliyopo Magharibi mwa Iran.

Urusi imekuwa ikifanya mashambulizi dhidi ya waasi nchi Syria kwa kutumia ngome yake iliyopo ndani ya Syria au kutokea Urusi kwenyewe. Lakini sasa imeanza kutumia ngome yake iliyopo nchini Iran.

Akizungumza kutoka Wizara ya Ulinzi ya Marekani Pentagon Msemaji wa Jeshi la Marekani Kanali Chris Garver amesema majeshi ya ushirika yamearifiwa kuhusu mpango huo Urusi.