Trump atetea Polisi kuhusu mauaji ya Milwaukee

Donald Trump amekuwa akikosolewa kwa kutoa matamshi yanayodaiwa kuwa ya kibaguzi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Donald Trump amekuwa akikosolewa kwa kutoa matamshi yanayodaiwa kuwa ya kibaguzi

Mgombea urais wa Marekani kupitia Chama cha Republican Donald Trump ambaye yupo katika mji Milwaukee amesema ushahidi wa awali unaonyesha kuwa ilikuwa ni halali kijana mweusi aliyeuawa na polisi katika mji huo siku ya jumamosi.

Mauaji ya kijana huyo Syville Smith ambayo yalitokea katika mji huo Milwaukee wenye wamarekani wengi wenye asili ya Afrika katika mji ulisababisha maandamano makubwa hivi karibuni.

Katika kampeni hiyo Trump amemshambulia mpinzani wake Hilary Clinton kwamba amechangia kuwepo kwa vurugu katika mji huo.

"Utekelezaji wa sheria, kujumuisha jamii , utendaji bora wa polisi ni mambo ambayo nchi yetu inahitaji.

Kama vile mgombea urais wa Hilary Clinton yeye alikuwa hawajali watu wa hali wa chini alikuwa anawapinga polisi mniamini mimi. Hayo yamekuwa yakihamasisha uhalifu kama ubaguzi kwenye jamii yetu mambo ambayo yamekuwa yakichochowa na mpinzani wangu ambaye ameshiriki moja kwa moja vurugu za Milwaukee na maeneo mengine katika nchi yetu." Alisema.