Kituo cha uhamiaji cha Australia kilichopo kisiwa cha Manus kufungwa

Peter O'Neill Waziri mkuu wa Papua New Guinea
Image caption Peter O'Neill Waziri mkuu wa Papua New Guinea

Serikali ya Australia na Papua New Guinea zimekubaliana kufunga kituo cha uhamiaji cha Australia kilichopo katika kisiwa cha Manus nchini Papua.

Tangazo hilo limetolewa kufuatia mazungumzo baina ya waziri ya Uhamiaji ya Australia, Peter Dutton na Waziri mkuu wa Papua New Guinea ,Peter O'Neill.

Image caption Wamekubaliana kukifunga kituo hicho mwezi Aprili

Wamekubaliana kukifunga kituo hicho mwezi Aprili, baada ya Nchi yake kutoa maamuzi kuwa watu waliowekwa kizuizini ilikuwa kinyume cha sheria na katiba.

Bwana Dutton amesema kuwa hamna hata mtu mmoja kati ya watu mia nane wanaokaa kwenye kituo watakopewa ardhi Nchini Australia.

Image caption Ramani ya eneo hilo