Semenya kushiriki mbio za mchujo leo

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Semenya aligunduliwa kuwa na kiwango cha juu cha chembechembe za kiume mwaka 2009

Mwanariadha wa Afrika Kusini Caster Semenya, hii leo atashiriki mbio zinazosubiriwa kwa hamu za mita 800 mchujo kwa akina mama.

Utata umekumba taaluma ya Semenya tangu anafanyiwe uchunguzi wa jinsia yake mwaka 2009, ambapo aligunduliwa kuwa na viwango vya juu vya chembe chembe za kiume.

Kabla ya kufanyika kwa mashindano ya olimpiki ya Rio, kulikuwa na maoni tofauti ikiwa Semenya angeweza kuruhusiwa kushiriki mbio za wanawake.

Anatarajiwa kushinda mbio hizo na hata kuvunja rekodi ya miaka 33.

Watu nchini Afrika Kusini wameingia kwenye mitandao ya kijamii kumtetea Semenya na hata kufikia kiwango cha kumtungia shairi.