Mtaalamu wa nyota anayewachochea wasichana kupenda sayansi

Haki miliki ya picha Daniel Chu/Travelling Telescope
Image caption Msichana akitazama angani kwa kutumia darubini

Mtaalamu mmoja wa nyota nchini Kenya, anasafiri pamoja na darubini yake katika maeneo ya mashambani nchini humo, kwa lengo la kuwachochea watoto wasichana kuyapenda mambo yanayohusu sayansi.

Mradi huo wa Susan Murabana una lengo la kujenga kituoa cha kwanza cha umma cha kutazana nyota.

Ana matumani kuwa mradi huo utabuni ajira kwa wanafunzi wa masuala ya sayansi nchni Kenya, na pia kuwavutia watu kutoka eneo lote la Afrika ya Mashariki.

Anasema kuwa bado watu hawajaelewa jinsi sayansi ya nyota inaweza kutumiwa katika nyanja zingine maishani.