Rais Magufuli aahidi kumnunulia mlemavu baskeli

Haki miliki ya picha TBC
Image caption Rais Magufu amehidi kuwa atamnunulia mlemavu huyu baiskeli ya magurudumu matatu

Rais wa Tanzania John Magufuli ameahidi kuwa atamnunulia baiskeli ya magurudumu matatu, mwanamme mmoja mwenye ulemavu, baada ya kumuona wakati wa matangazo ya habari akitumia kwa umahiri mkubwa baiskeli ya kawaida.

Katika taarifa iliyosomwa wakati wa matangazo ya habari, Rais Magufuli alisema kuwa atatumia pesa kutoka kwa mshahara wake mwenyewe kununua baiskeli hiyo na kumkabidhi mwanamme huyo baada ya juma moja.