Mabilioni ya fedha yafujwa Vyuo vikuu Tanzania

Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na mafunzo ya ufundi Profesa Joyce Ndalichako
Maelezo ya picha,

Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojia na mafunzo ya ufundi Profesa Joyce Ndalichako

Baada ya uhakiki wa miezi kadhaa kwenye vyuo vikuu nchini Tanzania taarifa mpya imeibainisha ufisadi mkubwa ndani ya vyuo vikuu ambapo mabilioni ya fedha za kitanzania zimepotea na kufujwa kwa malipo ya mikopo hewa ya maelfu ya wanafunzi ambao hawapo vyuoni.

Kufuatia ufisadi huo Serikali ya Tanzania sasa imetoa siku saba kwa vyuo vikuu vyote nchini humo vilivyopokea fedha za mikopo kwa wanafunzi hewa ambao hawapo vyuoni kuzirejesha serikalini mara moja.

Aidha pia imevipa agizo vyombo vya dola nchini humo kuanza mara moja kuwachukulia hatua za kisheria wote watakaobainika kuhusika na sakata hilo.