Mvulana aliyebaka India kuhukumiwa kama mtu mzima

Mabadiliko ya sasa yanatumika kwa matukio ya ubakaji Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mabadiliko ya sasa yanatumika kwa matukio ya ubakaji

Maafisa nchini India wamesema kuwa mvulana wa miaka anayetuhumiwa kwa kosa la kubaka, anapaswa kuhukumiwa kama mtu mzima.Hili ni kesi ya kwanza kuhamishwa na kupelekwa katika mahakama ya watu wazima juu ya makoa sa ya ubakaji hii ikichagizwa na mabadiliko ya sheria yaliyofanya mwaka jana.

Hapo awali watoto waliokumbwa na keshi ya kubaka wakiwa na miaka chini ya 18 wangeliweza kufungwa jela kifungo kisichozidi miaka mitatu.

Mabadiliko ya sasa yanatumika kwa matukio ya ubakaji na tiyari yamekwishatumika katika kesi za mauaji.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Sheria hii itatoa afueni kwa watoto wa kike na wanawake

Mvulana huyo anatuhumiwa kumbaka msichana wa miaka 17 ambaye ni mwanafunzi.