Wanamuziki wakabili unyanyasaji katika ndoa Kenya
Huwezi kusikiliza tena

Wanamuziki wakabili unyanyasaji katika ndoa Kenya kupitia muziki

Visa vya dhuluma katika ndoa vinazidi kuongezeka nchini Kenya, cha hivi karibuni kikiwa cha mwanamke aliyekatwa mikono yake miwili na mumewe, akidai kuwa, yeye ni tasa.

Kulingana na takwimu, zaidi ya asilimia 38.2 ya wanawake huaathiriwa na dhulma hizo,ikilinganishwa na asilimia 21 ya wanaume wanaokabiliwa na dhulma hizo.

Kama njia mojawepo za kuhamasisha jamii kuhusu tatizo hilo, bendi maarufu ya wanamuziki kutoka Kenya wametunga wimbo, "sirudi" unaowahimiza waathiriwa kuzungumzia shida zao na pia kujiondoa dhuluma zikizidi.

Mkakati huo tayari umepata mafanikio kama anavyotuarifu Anthony Irungu.