Umoja wa Mataifa chanzo cha Kipindu pindu Haiti

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon
Image caption Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon

Umoja wa mataifa umekiri kuwa ulichangia mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu miaka sita iliyopita ulioua watu zaidi ya elfu kumi nchini Haiti.

Taarifa za kisayansi zinaonyesha Majeshi ya Umoja wa Mataifa kutoka Nepal ndio waliokuwa chanzo cha ugonjwa huo jambo ambalo limekuwa likipingwa na Umoja huo wa Mataifa.

Ripoti ya ndani iliyoonekana na gazeti la New York Times sasa imefanya Umoja huo ubadilike.

Taarifa hiyo imemalizia kuwa ugonjwa huo usingelipuka lakini kwa matendo ya Umoja wa mataifa na hatua iliyochukuliwa ilikuwa si kuzingatia uzito na yenye kujihami. Hata hivyo Umoja wa Mataifa umendelea

kung'angania kuhusu uhalali wake wa kisheria kwamba unalindwa sheria za kidiplomasia kwamba hawawezi kulipa walioathirika.