Wanaharakati wapinga utumwa nchini Mauritania

Wamekuwa wakiandamana kupinga kuwalazimisha wakazi kuhama kutoka eneo lenye mazingira magumu katika mkuu Nouakchott
Image caption Wamekuwa wakiandamana kupinga kuwalazimisha wakazi kuhama kutoka eneo lenye mazingira magumu katika mkuu Nouakchott

Wanaharakati kumi na watatu wa kupinga utumwa nchini Mauritania wamehukumiwa kifungo gerezani kufuatia kijihusisha na maandamano mwezi june ambayo yalipelekea kuibuka kwa vurugu.

Wapiga kampeni hao wa shirika lisilo la kiserikali la kupambana na utumwa lenye makao makuu yake Biram Dah Abeid nchini Mauritania wamepewa hukumu hiyo ya kati ya miaka mitatu hadi kumi na mitano kufuatia mashtaka ya uasi, mikusanyiko ya silaha na kuwa wanachama wa shirika lisilo halali.

Wamekuwa wakiandamana kupinga kuwalazimisha wakazi kuhama kutoka eneo lenye mazingira magumu katika mkuu Nouakchott.

Wanaharakati hao wanasema watu ambao ni watoto wa watumwa weusi,bado wanaishi kwa masharti kutokea akim hadi bondage.

Maafisa wa Mauritania walipiga marufuku utumwa tangu mwaka 1981.