Taliban wateka wilaya muhimu nchini Afghanistan

Wapiganaji wa Taliban waliinga mji wa Kunduz mwezi Septemba Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wapiganaji wa Taliban waliingia mji wa Kunduz mwezi Septemba

Wanamgambo wa Taliban wameteka wilaya muhimu katika mkoa ulio kaskazini mwa Afghanistan wa Kunduz.

Wapiganaji hao walishambulia kutoka sehemu tofauti hatua iliyowalazimu wanajeshi wa serikali kurudi nyuma kwenda mji wa Kunduz.

Ukosefu wa risasi na vikosi zaidi vilichangia kutekwa kwa wilaya ya Khanabad.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wanajeshi wa serikali wanasema kuwa waliishiwa na risasi

Taliban wamepiga hatua tangu vikosi vya kimataifa visitishe shughuli zao mwaka nchini Afghanistan 2014.

Wanajeshi wa Afghanistan kwa sasa wanapigana na wanamgambo hao walio karibu nusu ya wilaya zote 34 nchini humo

Mapema wiki hii Taliban walitaka wilaya moja iliyo mkoa jirani wa Baghlan.