Ndege ndefu zaidi hatimaye yapaa Uingereza

Huwezi kusikiliza tena
Wakati Airlander 10 ilipaa kutoka uwanja Cardington

Safari ya ndege ndefu zaidi dunian imeanza nchini Uingereza baada ya majaribio ya awali kufutwa dakika za mwisho.

Ndege hiyo inayojulikana kama Airlander 10, ambayo ni ndege na pia meli, ilitoka uwanja wa Cardington huko Bedfordshire.

Ndege hiyo ya gharama ya pauni milioni 25 ina urefu wa mita 93, ni refu kwa mita 15 zaidi ya ndege yoyote kubwa ya abiria.

Huwezi kusikiliza tena
Picha iliyochukuliwa kutoka kwa helkopta ikionyesha Airlander 10

Ndege hiyo hairuhusiwi kuruka usiku inapofanyiwa majaribio.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Airlander 10 - ambayo imeundwa kama ndege na meli - ilipaa kutoka uwanja waCardington Airfield huko Bedfordshire
Haki miliki ya picha South Beds News Agency
Image caption The Airlander 10 was originally designed for long-range surveillance for the US Government

Ndege hii iliundwa kwanza kwa serikali ya Marekani kama ndege ya kufanya ujasusi lakini mradi huo ukafutwa kutokana na ukosefu wa fedha.

Kisha kampuni ya uingereza ya Hybrid Air Vehicles (HAV) ikazindua kampeni ya kufanikisha mradi huo.

Ndege hiyo ina uwezo wa kusalia angani kwa takriban siku tano.

Kampuni ya HAV inasema ndege hiyo itatumiwa kwa masuala kadhj yakiwemo ujasusi, mawasiliano, kusafirisha misaada na hata abiria.