Watu waliokuwa wakiandamana washambuliwa Yemen

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu waliokuwa wakiandamana washambuliwa Yemen

Mabomu yanaripotiwa kudondoshwa karibu na umati mkubwa wa watu waliokuwa wakiandamana katika mji mkuu wa Yemen Sanaa.

Maelfu ya watu walikuwa wamekusanyika kupinga mashambulizi ya hivi majuzi yanayofanywa na muungano unaongozwa na Saudi Arabia unoependelea serikali iyoungwa mkono kimataifa.

Hakuna taarifa zilizothibitishwa kuhusu majeruhi.

Saudi Arabia imelaumiwa mara kwa mara na makundi ya kutetea haki za binadamu kutokana na vifo vinavyowakumba raia vinavyosababishwa na mashambulizi yake.

Watu 19 waliuawa wakati hospitali moja iliyo kaskazi mwa nchi ilishambuliwa siku ya Jumatatu.