Serikali ya Ufilino na wapiganaji wapata makubaliano

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Rais Duterte anataka kumaliza mapambano ya muda mrefu zaidi nchini Ufilipino

Serikali ya Ufilipino na wapiganaji wa Kikoministi, wamekubalina kusitisha mapigano, kabla ya mazungumzo ya amani yatakoyofanywa Norway juma lijalo.

Makubaliano yanatarajiwa kuanza kutekelezwa hapo kesho.

Mshauri wa serikali, Jesus Dureza, alisema mapigano yatasita kwa muda unaohitajika.

Rais Rodrigo Duterte alimaliza usitishwaji wa mapigano mwezi uliopita, kwa sababu kundi la Kikoministi la NPA, nalo halikusitisha mapigano katika muda alioweka.

Hayo ni mapambano ya muda mrefu nchini Ufilipino, ambayo Rais Duterte anataka kuyamaliza.