Barua pepe: Jaji amtaka Clinton kujibu mashtaka

Hillary Clinton
Image caption Hillary Clinton

Jaji mmoja wa Marekani amesema kuwa mgombea wa urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton lazima ajibu mashtaka yanayomkabili kuhusiana na matumizi mabaya ya barua pepe kwa maandishi kuelezea hali ilivyokuwa alipokuwa waziri wa maswala ya kigeni.

Kundi moja la wakereketwa wasiopendelea mabadiliko, Judicial Watch, limeishtaki wizara ya mashauri ya kigeni juu ya swala hilo likimtaka bi Clinton kutoa ushahidi binafsi chini ya kiapo.

Shirika la upelelezi la FBI lilikamilisha uchunguzi wake katika barua pepe hizo mwezi uliopita, bila kupendekeza mashtaka yo yote dhidi ya bi Clinton.

Mada zinazohusiana