Watu 15 wauawa kwa mlipuko wa bomu nchini Somalia

Milio ya risasi ilisikika wakati wa makabiliano na polisi
Image caption Milio ya risasi ilisikika wakati wa makabiliano na polisi

Milipuko miwili ya mabomu iliyotekelezwa na kundi la kigaidi la Alshabab imesababisha vifo vya watu 15 katika mji wa Galkayo.

Magari mawili yaliyoliwekwa mabomu hayo yaliegeshwa mbele ya makao makuu ya serikali ya mtaa.

Milio ya risasi ilisikika wakati wa makabiliano na polisi.

Meya wa mji huo amesema jaribio la kuteka majengo mbalimbali limeshindikana.

Ni shambulio la pili ndani ya kipindi cha miezi sita katika mji huo ambao haujaathiriwa na machafuko kama sehemu nyingne za nchi ya Somalia.

Mwezi wa tatu mshambuliaji alivamia hoteli katika mji huo wa Galkayo na kusababisha vifo vya watu sita akiwemo afisa wa serikali.