Shambulizi la Uturuki limefanywa na kijana wa miaka 14 pekee

Linatajwa kuwa shambulizi lililouwa watu wengi zaidi nchini Uturuki mwaka huu
Image caption Linatajwa kuwa shambulizi lililouwa watu wengi zaidi nchini Uturuki mwaka huu

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amesema kuwa shambulizi la bomu la kujitoa muhanga lililofanywa siku ya jumamosi katika mji wa Gaziantep lilifanywa na mtu anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 12 na 14.

Erdogan amesema anaamini kuwa wapiganaji wa kundi la la Islamic State huenda wakawa wametekeleza shambulizi hilo, ambalo limeuwa zaidi ya watu 50 waliokuwa kwenye harusi ya kikudishi.

Linatajwa kuwa shambulizi lililouwa watu wengi zaidi nchini Uturuki mwaka huu.

Image caption Shambulizi hilo limeuwa zaidi ya watu 50

wapiganaji wa IS wamepoteza ardhi katika Jirani na Kaskazini mwa syria.

Ripoti zinasema kuwa waasi wanaoisaidia Uturuki wanajiandaa kukabiliana nao katika mipaka kati ya nchi hizo mbili.