Muhtasari: Habari kuu leo Jumatatu

Miongoni mwa habari kuu hivi leo, michezo ya Olimpiki ya Rio imefungwa rasmi leo na maelfu ya watu wameandamana kupinga pendekezo la kubinafsisha mpango wa hazina ya malipo ya uzeeni.

1. Sherehe za kusisimua kufunga michezo ya Olimpiki Rio

Haki miliki ya picha AFP

Sherehe za kufunga rasmi mashindano ya Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu wa 2016, huko Rio De Jeneiro, nchini Brazili, zimefanyika usiku wa kuamkia leo. Sherehe hizo sawa na zile za ufunguzi, zimefanyika katika uwanja wa Maracanna, ambapo utengano wa kila timu ulivunjwa rasmi, baada ya washiriki wa Olimpiki kwa pamoja waliingia na kucheza uwanjani. Rais wa kamati kuu ya Olimpiki IOC, Tomas Bach, alihutubu kwa lugha ya kiingereza, Kifaransa na Kireno, huku akiwaambia wanaridha kuwa, wameonyesha nguvu ya michezo kama kiunganishi kikuu Duniani.

2. Tokyo yakabidhiwa bendera ya Olimpiki

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Gavana wa Tokyo Yuriko Koike akipokea bendera ya Olimpiki

Bendera ya Olimpiki imekabidhiwa mwenyeji wa mashindano ya Olimpiki mwaka 2020, mjini Tokyo, Japan.Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, alikuwepo mwenyewe akiwa amevalia mavazi sawa na kibonzo wa Sinema, kwenye mchezo wa Video -Super Mario, ulioundiwa nchini Japan.

3. Polisi watwaa hati za kusafiria za maafisa wa Ireland Brazil

Haki miliki ya picha PA
Image caption Maafisa hao watatu wametakiwa kujisalimisha kwa polisi

Polisi nchini Brazil, wanasema kuwa wamechukua hati ya kusafiria za maafisa watatu wa baraza kuu la Olimpiki kutoka Ireland, kama sehemu ya uchunguzi ya uuzaji haramu wa tiketi za kutizama mashindano hayo.

Sasa wanahojiwa leo Jumatatu. Jaji mmoja mjini Rio, aliamrisha kutwaliwa kwa hati hizo za kusafiria za maafisa wengine watatu zaidi wa Olimpiki.

4. Maelfu washiriki maandamano Chile

Haki miliki ya picha AP
Image caption Maandamano hayo yalifanyika bila vurugu, polisi wamesema

Mamia kwa maelfu ya watu kote nchini Chile wanashiriki katika maandamano makubwa, kupinga kubinafsishwa kwa mpango wa mafao ya uzeeni.

Waandamanaji wanasema kuwa mamilioni ya watu, waliojiunga na mpangop huo baada ya mwaka 1981, kwa sasa wameachwa na kipato cha chini mno cha uzeeni.

5. Uingereza kuchukua hatua dhidi ya mahabusu wenye itikadi kali

Haki miliki ya picha PA

Waziri wa haki na sheria nchini Uingereza, Liz Truss, atatangaza hatimaye leo Jumatatu, hatua mpya ya kuzuia mahabusu wa Kiislamu waliofungwa kuendelea kutoa mafunzo ya itikadi kali kwa wafuingwa wengine. Uchunguzi umependekeza kuwa, wafungwa hao walio na mafunzo ya itikadi kali, kuzuiliwa ndani ya vizuizi vya kipekee, mbali kabisa na wafungwa wengine.

6. Ndege za Israel zashambulia Beit Hanoun

Duru za kijeshi nchini Israeli, zinasema kuwa, ndege zake na vifaru zimesambaratisha kabisa mji wa Beit Hanoun, kaskazini mwa ukanda wa Gaza, katika hatarakati za kujibu shambulio la roketi, lililotekelezwa na wanamgambo wa Kipalestina.

Roketi hiyo iliangushwa katika mji wa Sderot, nchini Israeli, lakini haikusababisha maafa yoyote au uharibifu.