Mtindo wa kuvalia magome ya miti Uganda

Mtindo wa kuvalia magome ya miti Uganda

Nchini Uganda kumekuwa na ubunifu wa kipekee ambao umekuwa ukitumika kutengeneza vitambaa kwa karne chungu nzima nchini humo.

Nguo zinazotengenezwa kwa kutumia magome ya miti huvaliwa katika sherehe za jadi, ingawa matumizi ya nguo hizi yamepungua zaidi miaka ya hivi karibuni.

Wabunifu wa mavazi nchini Uganda kwa sasa wanajaribu kulipa tena umaarufu vazi hilo la jadi kwa kutumia aina za kisasa.

Ifuatayo ni taarifa ya Nancy Kacungira.