Muanzilishi wa bendi za Backstreet Boys na NSYnc afariki

Lou Pearlman Haki miliki ya picha AP
Image caption Pearlman alifungwakifungo cha miaka 25 years mwaka 2008

Mwanzilishi wa bendi ya Boy Band, Lou Pearlman amefariki akiwa na umri wa miaka 62 .

Pearlman ndio mwazilishi wa bendi ya Backstreet Boys,bendi maarufu iliosajili mauzo mengi pamoja na ile ya NSYnc ,miongoni mwa bendi nyenginezo.

Alifungwa kwa takriban miaka 25 mwaka 2008 kwa kuhusika na udanganyifu wa mpango wa Ponzi uliogharimu dola milioni 300.

Mwambaji wa NSYnc Lance Bass alituma ujumbe katika Twitter akisema kuwa Pearlman hakuwa mfanyibiashara mzuri lakini hangekuwa pale alipo bila ushawishi wake.

"habari ni kwamba #LouPearlman amefariki.Hakuwa mfanyibiashara mzuri ,lakini sidhani nisingekuwa nikifanya kitu ninachokipenda sana bila ushahwishi wake.Pumzika kwa amani Lou''.

Sababu ya kifo chake bado haijulikani.

'Ulafi ulimtawala'.

Pearlman alivutiwa na ufanisi wa bendi ya New Kid on The Block na kuanzisha kampuni yake ya kurekodi ambapo alizindua bendi ya vijana wenye vipawa kwa Jina Backstreet Boys.

Bendi hiyo iliuza vibao milioni 130.NSync pia walifanikiwa pakubwa na kuweza kuuza vibao milioni 55.

Image caption Bendi ya Backstreet Boys

Pearlman baadaye aliongoza bendi nyengine za vijana kama vile LFO, Take 5, Natural na O-Town, na kundi la wasichana, lililoshiriki katika wimbo wa mwanamuziki Britney Spears.

Pearlman alidanganya familia , marafiki , wawekezaji na benki kwa kuwashawishi kuwekeza fedha zao kwenye kampuni bandia kwa takriban miaka 20.

Mada zinazohusiana