Kwa Picha: Waafrika wanaoishi India

Hamza & Shukura, Nigeria
Image caption Hamza and Shukura from Nigeria, living in Jaipur, India

Mwezi wa Januari mwana huu, mwanafunzi kutoka Tanzania alidhalilishwa kwa kuvuliwa nguo na umati wa watu katika jiji la Bangalore, kusini mwa India, baada ya gari la mwanafunzi kutoka Sudan kumgonga na kumuua mwanamke mmoja eneo hilo.

Mpiga picha Mahesh Shantaram, alishangazwa na kisa hicho na visa kama hivyo kwa Waafrika nchini India na akaanza kuyaangazia maisha ya Waafrika hao.

Shantaram alianza upigaji picha hizo kutoka Bangalore, na hata kwa miji mengine kama vile Jaipur, Delhi na Manipal akiangazia wanafunzi ambao walikuwa wachache .

Msururu wa picha zao ni sehemu mojawepo ya maonyesho yanayoandaliwa na Tasveer.

"Kila picha ina jukumu lake la kuonyesha jinsi Waafrika wanavyoishi nchini India kwa kuweka picha za upweke, hisia ya uadui, na ukosefu wa nafsi," alisema mtaalam wa sanaa Caroline Bertram, katika makala maalum ya maonyesho hayo.

Image caption Ola na Jason kutoka Nigeria, wanaoishi Delhi
Image caption Abdul-Kareem kutoka Nigeria, anayeishi Jaipur
Image caption Vitu kutoka Malawi, anayeishi Bangalore
Image caption Charity na rafiki zake kutoka South Africa, wanaoishi Manipal
Image caption Ameenou kutoka Nigeria, anayeishi Jaipur
Image caption Misana kutokaTanzania, anayeishi Bangalore
Image caption Prosper kutoka Tanzania, anayeishi Bangalore
Image caption Wandoh kutoka Chad, anayeishi Bangalore