Watu 40 wajeruhiwa kwa gesi nchini Bangladesh

Waathiriwa wamepata tatizo la kupumua baada kuvuta gesi hiyo
Image caption Waathiriwa wamepata tatizo la kupumua baada kuvuta gesi hiyo

Karibu watu 40 wamelazwa hospitali huko Bangladesh baada ya gesi kuvujia katika kiwanda cha mbolea mjini Chittagong.

Wengine wapo katika hali mbaya.

Waathiriwa wamepata tatizo la kupumua baada kuvuta gesi hiyo.

Watu wa maeneo hayo wamehamishiwa sehemu zenye usalama wa afya ya zao.

Magari kumi ya zimamoto yanafanya jitihada ya kuzuia kuvuja kwa gesi hiyo.