Akhwari: Mtanzania aliyetukuka Olimpiki Mexico
Huwezi kusikiliza tena

Akhwari: Mtanzania aliyetukuka Olimpiki Mexico

Akijulikana kwa tukio la 'Nafasi ya Mwisho Iliyotukuka' katika mashindano ya Olimpiki, John Stephen Akhwari anakumbukwa duniani kote kwa Michezo ya Olimpiki ya mwaka 1968 iliyofanyika nchini Mexico.

Ilikuwa imepita zaidi ya saa moja tangu wakimbiaji wote katika mashindano hayo wakiwa wamewasili katika mstari wa mwisho, mara kijana mmoja mkimbiaji akaingia uwanjani akiwa amevaa sare zenye bendera ya Tanzania huku akichechemea.

Miguu yake ikiwa na majeraha yaliyofungwa bendeji, waandishi wa habari walimzunguka kisha mmoja akamuuliza "John, kwanini hukuacha kukimbia wakati ulijua kabisa kwamba huna nafasi ya kushinda?"

Naye akamjibu "Nchi yangu haikunituma kuanza mashindano bali kuyamaliza" .

Leo hii akiwa na umri wa miaka 78, Mwandishi wetu Sammy Awami alikwenda kumtembelea kijijini kwao Mbulu, Kaskazini mwa Tanzania na haya hapa ndio mahojiano yao.