Mpiga tarumbeta wa Bob Marley, afariki

Headley Bennett
Image caption Headley Bennett

Mpiga tarumbeta Headley Bennett, ambaye alishiriki katika wimbo wa kwanza wa mwanamuziki maarufu wa nyimbo za rege Bob Marley 'Judge Not,' amefariki akiwa na umri wa miaka 85.

Mwanawe Carol Bennett, alithibitisha kifo cha mwanamuziki huyo siku ya Jumapili.

Carol hakusema sababu maalum ya kifo cha mwanamuziki huyo, lakini alisema babake alikuwa akiugua shinikizo la damu na hivi majusi alipatika na saratani ya kiume.

Haki miliki ya picha BBC/Getty Images
Image caption Bennett alishiriki kwa muziki wa Gregory Isaacs na Jimmy Cliff

Benneth alishiriki na wanamuziki wa nyimbo za rege kama vile Bunny Wailer na Gregory Isaacs.

Alituzwa na serikali ya Jamaica mwaka wa 2005 kama Mjamaica wa sita mwenye hadhi ya juu.