Mwanamume ameza visu 40 nchini India

Visu vilivyotolewa tumboni Haki miliki ya picha CORPORATE HOSPITAL
Image caption Visu vilivyotolewa tumboni

Madaktari katika mji wa Amritsar kaskazini mwa India wamesema, wametoa visu 40 kutoka kwa tumbo la mwanamume mmoja.

Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 42 alikuwa amevimeza visu hivyo kwa muda wa miezi mitatu.

Daktari Jatinder Malholtra, ameambia BBC kwamba alikutana na mwanamume huyo wiki iliyopita alipokuwa akihisi maumivu makali kwenye tumbo lake.

Alisema mwanamume huyo hakuwafahamisha madaktari hao kwamba alikuwa akimeza visu.

Haki miliki ya picha CORPORATE HOSPITAL
Image caption Picha za visu hivyo kwenye tumbo

'Tuligundua mwanamume huyo alikuwa akitafuna visu baada ya kumfanyia uchunguzi .'Dkt. Malholtra alisema.

Mwanamume huyo anaendelea kupata nafuu na yuko katika hali dhabiti.

Operesheni hiyo iliwahusisha madaktari watano na ilichukua saa tano kukamilika

Kwa sasa madaktari hao wanajaribu kutafuta sababu ya mwanaume huyo kumeza visu hivyo.

Mada zinazohusiana