Mwanajeshi apigwa risasi na kufariki katika zoezi Uskochi

Kambi iliyotumika na wanajeshi tangu mwaka 1911 Haki miliki ya picha Google
Image caption Kambi iliyotumika na wanajeshi tangu mwaka 1911

Mwanajeshi mmoja amefariki baada ya kupigwa risasi katika eneo la kambi ya mafunzo ya Northumberland iliyoko kaskazini mwa Uingereza.

Mwanajeshi huyo wa kiume ambaye alikuwa akitumikia kwenye kikosi cha mfalme wa Ukochi, alipigwa risasi katika maeneo ya kambi hiyo ya Otterburn katika zoezi la ufyatuliaji wa risasi mwendo wa saa nane.

Polisi wa Northumbria amesema mwanajeshi huyo alipata 'majeraha mabaya ya kichwa' na kutangazwa kufariki papo hapo.

Haki miliki ya picha MARK OWENS/ARMY HQ SCOTLAND
Image caption Wanajeshi wa Scotland

Hatahivyo bado mwanajeshi huyo hajatambuliwa na Wizara ya Ulinzi nchini humo.

Waziri wa majeshi Mike Penning amesema: 'Mafikira yake yako kwa familia, jamaa na marafiki wa mwanajeshi huyo haswa wakati huu mgumu'.

Eneo la mafunzo la Otterburn , lilibuniwa na waziri mkuu wa zamani Sir Winston Churchill , na ni sehemu kubwa ya pili nchini humo iliyotengwa kwa wajeshi kufanyia mazoezi ya ufyatuliaji wa risasi tangu mwaka 1911