Malipo ya akinamama wanaojifungua yameendelea kuwa chini ya wanaume

Malipo ya wanawake Haki miliki ya picha PA
Image caption Kwa wastani wanawake , hulipwa silimia 18% chini ya wanaume kwa saa, kwa mujibu wa utafiti wa IFS.

Wanawake wanaorejea kazini kufanya kazi ya muda baada ya kupata watoto huendelea kupata malipo ya chini kuliko wanaume kwa miaka mingi baadae, imesema ripoti ya Taasisi ya Mafunzo ya Mapato (IFS).

Pengo la mapato baina ya wanaume na wanawake limeendelkea kuwa pana zaidi katika miaka ya baada ya kuzaliwa kwa mtoto, taasisi ya IFS imesema.

Wanawake wamekosa kupewa vyeo kazini na kupata uzoefu mdogo kikazi kuliko wanaume, suala ambalo linawazuia kupata mamlaka, iliongeza ripoti hiyo.

Katika kipindi cha miaka 12 mfulurizo, pengo hilo liliongezeka kwa asilimia 33% ikilinganishwa na viwango vya malipo ya wanaume kwa saa.

Robert Joyce, mmoja wa waandishi wa IFS wa ripoti hiyo, amesema wanawake hawakuweza kuona mara moja kupunguzwa kwa mapato yao ya kila saa walipopunguza saa zao za kazi baada ya kujifungua.

"badala yake , wanawake wanaofanya kazi nusu ya muda wa kazi hupoteza mapato yao mfulurizo, hii ikimaanisha kuwa malipo ya kila saa ya wanaume (na ya wanawake kwa muda kamili wa kazi) huwa ya juu sana zaidi yao.

Haki miliki ya picha PA
Image caption Baada ya kurejea kazini kufuatia kujifungua mtoto wa kwanza, tofauti ya malipo ya mshahara kwa saa huongezeka sana.

"zaidi ya hayo , wanawake wanaosimamisha kazi za malipo na baadae kurejea katika soko la ajira hupata hasara katika ukuaji wa malipo ,"aliongeza.

Wanaume wana uwezekano wa kupandishwa vyeo kazini kwa asilimia 40% zaidi ya wanawake na kuingia katika ngazi za utawala , ulibaini utafiti mwingine.

Kwa wastani wanawake , hulipwa silimia 18% chini ya wanaume kwa saa, kwa mujibu wa utafiti wa IFS.

Baada ya kurejea kazini kufuatia kujifungua mtoto wa kwanza , tofauti ya malipo ya mshahara kwa saa huongezeka sana.